Tuesday, March 7, 2017

Magufuli azindua uwanja wa ndegevita Tanzania

Rais Magufuli akifyatua risasi hewani kuashiria ufunguzi wa uwanja wa ndege vita nchini TanzaniaHaki miliki ya pichaIKULU YA TANZANIA
Image captionRais Magufuli akifyatua risasi hewani kuashiria ufunguzi wa uwanja wa ndege vita nchini Tanzania
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amezindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere uliofanyiwa ukarabati baada ya miundombinu ya uwanja huo kuharibika.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Tanzania (JWTZ) kwa kazi kubwa linayofanya na pia akamshukuru Rais wa China Xi Jinping na Serikali yake kwa msaada mkubwa iliyoutoa kujenga uwanja huo.
  • "Mhe. Balozi Lu Youqing naomba unipelekee shukrani zangu za dhati kwa Rais wa China kwa kutoa msaada huu mkubwa wa kujenga uwanja wa ndegevita wa Ngerengere, najua China imetusaidia kujenga Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki na Uwanja wa Mpira, hii yote inathibitisha uhusiano wetu mzuri, urafiki na undugu

0 comments:

Post a Comment